Simon Sirro IGP mpya Tanzania

Ernest Mangu

Serikali ya Tanzania imemteua Kamishna wa Polisi Simon Sirro kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).

Kabla ya uteuzi huo Sirro alikuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Sirro anachukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Sirro, kwa mujibu wa ratiba ya Ikulu, ataapishwa Jumatatu saa mbili na nusu Ikulu Jijini Dar es Salaam.