Hali ya tahadhari kwenye mpaka wa Serbia na Kosovo

Polisi akiwa amesimama karibu na gari linalocheka kwa moto kufuatia makabiliano kati ya waandamanaji na polisi wa Kosovo May 26, 2023

Wanajeshi wa Serbia walio kwenye mpaka na Kosovo, wamekuwa katika hali ya tahadhari ya juu kuanzia Ijumaa, baada ya kutokea makabiliano kati ya polisi na watu wa Serbia, yaliyopelekea watu 10 kujeruhiwa.

Watu wa Serbia wanaoishi Kosovo waliandamana mitaani kuwazuia mameya wa Albania, kuingia ofisini.

Makabiliano yalitokea baada ya polisi wa Kosovo kujaribu kuwaondoa waandamanaji ili kuwaruhusu wanasiasa hao kuingia ofisini.

Maafisa wamesema kwamba polisi watano wamejeruhiwa katika makabiliano hayo ya Ijumaa na magari kadhaa kuchomwa moto.

Uingereza, Ufaransa, Italy, Ujerumani na Marekani zimetoaa taarifa ya pamoja kuitaka Kosovo kumalizaa uhasama huo.

Rais wa Serbia Aleksandar Vucic amesema kwamba watalinda amani lakini Serbia haitakaa kimya pale ikiwa kutokea mashambulizi dhidi ya raia wa Serbia wanaoishi kaskazini mwa Kosovo.