Afrika kusini imetangaza janga la kitaifa baada ya mvua kubwa kukumba majimbo saba kati ya majimbo yote tis ana kusababisha mafuriko, uharibifu wa barabara, daraja na mimea shambani.
Idhara ya huduma ya dharura imetabiri kwamba mvua kubwa itaendelea kunyesha.
Taarifa kutoka ofisi ya rais imesema kwamba serikali imetangaza janga la kitaifa ili kuhakikisha kwamba kuna mikakati ya kutosha kukabiliana na mafuriko.
Taarifa hiyo hata hivyo haijasema iwapo kuna vifo vimetokea kutokana na mafuriko hayo.