Wafaransa washiriki katika uchaguzi muhimu wa rais

Mpiga kura akichukua vyeti vya kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais Ufaransa mjini Marseille, May 7, 2017.

Mgombea kiti cha rais  Marine Le Pen akiondoka nyumbani kwake Henin Beaumont, ona kurudi Paris baada ya kupiga kura yake. May 7, 2017.

Wapiga kura katika kituo cha kura mjini Lyon katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais. May 7, 2017.

Mgombea huru mwenye msimamo wa wastani Emmanuel Macron aakiondoka kutoka kituo cha kupiga kura cha Le Touquet, May 7, 2017.

wafaransa wasubiri kupiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi katika kituo cha Bron, May 7, 2017.

Wapiga kura wakaribishwa kwa kupewa mikate na keki walipowasili katika shule ya sekondari ya  Francais Charles de Gaulle katika mtaa wa South Kensington jijini London, May 7, 2017.

Usalama uko katika hali ya juu wakati wafaransa wanapiga kura katika uchaguzi wa kihistoria. May 7, 2017.

Bendera ya Ufaransa ikipeperushwa wakati wapiga kura wanawasili kupiga kura zao mjini Le Touquet, May 7, 2017.

Ukaguzi wa mikoba kabla ya kuingia ndani ya kituo cha kupiga kura mjini Paris, May 7, 2017.

Mwanamke akipiga picha wapiga kura wahamiaji huko Canada wanaosubiri kupiga kura wakati kuna mvua mjini Montreal, Quebec, Canada, May 6, 2017.