Besigye anyimwa nafasi ya malalamishi, Uganda

Dkt Kiiza Besigye aliegombea urais kwa chama cha FDC nchini Uganda.

Chama kikuu cha upinzani nchini Uganda cha Forum for Democratic Change, FDC, kinataka tume huru ya wakaguzi kuundwa ili kufanya uchunguzi wa kina wa jinsi uchaguzi mkuu ulivyofanyika nchini humo.

Your browser doesn’t support HTML5

Uchaguzi Uganda.

Haya yanajiri baada ya polisi kuwazuilia wakuu wa chama hicho pamoja na Dkt Kiiza Besigye aliekuwa mgombea wake wa urais, kufika mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita na ambao ulimpa Rais Yoweri Museveni ushindi.