Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo - FARDC kwa kushirikiana na kikosi cha ulinzi wa amani cha Umoja wa Mataifa - MONUSCO wamekubaliana kuimarisha nguvu zao ili kuwasaka na kuwanasa waasi wa kundi la FDLR kutoka Rwanda ambao wanasadikiwa kufanyia operesheni zao kwenye misitu ya Congo.
Msemaji wa jeshi la Congo katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Kapteni Njike ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Goma na kubainisha kuwa operesheni hiyo ya pamoja itahusisha kuwasaka waasi katika mkoa wote wa Kivu Kaskazini ikiwemo wilaya zza Rutchuru, Masisi na Walikale na sehemu moja ya Lubero.
Your browser doesn’t support HTML5
FARDC and MONUSCO kufanya operesheni ya pamoja
Naye msemaji wa MONUSCO nchini Congo ameyataka makundi yote ya waasi kusalimisha silaha zao na kuachana na viongozi wa makundi hayo ambayo yanaendelea kutenda uhalifu dhidi ya raia.