Waasi washambulia tena DRC.

Wakazi wa mji wa Beni, DRC wakiandamana kupinga mauwaji dhidi ya Kanali Ndala Januari 2013.

Watu wawili wamefariki Dunia wakati wa mapigano kati ya Jeshi la
Serikali ya Congo FARDC, na waasi wanao dhaniwa kuwa wa ADF kutoka
Uganda walio katika misitu ya Beni Kaskazini mashariki mwa Congo.

Your browser doesn’t support HTML5

Mapigano DRC.

Mapigano hayo yalitokea katika eneo la Opira Jumamosi usiku kaskazini mwa Mji wa Beni. Waasi hao wamekuwa wakishambulia kambi za jeshi la Congo na
vile vile makazi ya raiya.