Corona yasababisha watu kubadili tabia zao za kila siku

Waislamu katika miskiti wa Al Akbar mjini Surabaya, Indonesia wanasali wakiwa wamejiweka mbali mbali wakati wa sala ya Ijuma, ingawa katika sheria za kusali katika uislamu waumini wanahitajika kusali wakiwa bega kwa bega.

Watu katika train ya usafiri wa umaa katika mji wa Buenos Aires, Argentina wanava maski za uso kujikinga kutokana na kuenea kwa virus vya corona ingawa waatalamu wanashauri kamba watu wasio wagonjwa hawana haja ya kuva. 

Mjini Bangkok, Thailand mwanamke anasimama ndani ya lifti katika mahala iliyowekwa alama watu kutokaribiana katika jengo la maduka ili kupambana na COVID-19. 

Watu mjini Potsdam Ujerumani wasubiri kuingia katika duka la chakula la Rewe wakiwa wamesimama nyuma ya mstari mwekundu ili wasikaribiane.

Wanawake wawili wajiweka mbali na mbali wakizungumza katika bustani kati kati ya mji wa York Uingereza kaskazini. hii yote ni kwa sababu ya COVID-19.

Wanunuzi wasimama mbali na mbali katika mistari kuingia duka la chakula mjini Rome.
 

Wabunge wajiweka mbali na mbali ia wakati wa mkutano kujadili mswada kuhusu namna ya kupambana na corona nchini, katika bunge la Marekani mjini Washington.

Duka la kahawa limetengeneza boxing ya kuweka kahawa na kuwapatia wateja kwa kuvuta kamba ili wasikaribiane mjini Bangkok Thailand, wakati huu wa janga la COVID-19.

Watu wanakaa mahala ambapo pamewekwa alama nyekundu ndani ya treni ya mjini katika juhudi za kuto karibiana katika mji wa Palembang, Sumatra kusini, Indonesia.

Watu wasimama katika maeneo yaliyowekwa alama katika mgahawa mjini London, Uingereza.