Chama tawala cha ki-Conservative cha Waziri Mkuu wa Japan Shigeru Ishiba, kinajitayarisha kupunguza wingi wake katika uchaguzi wa leo Jumapili wa baraza kuu la bunge huku kukiwa na hasira za umma juu ya kashfa za kifedha za chama hicho na kutoridhika na uchumi ulioyumba.
Matokeo hayo yanaweza kudhoofisha nguvu ya Ishiba, na pengine kusababisha Japan kuingia katika hali ya sintofahamu ya kisiasa, ingawa mabadiliko ya serikali hayakutarajiwa.
Ishiba aliingia madarakani Oktoba 1, akichukua nafasi ya mtangulizi wake, Fumio Kishida, ambaye alijiuzulu baada ya kushindwa kuwatuliza wananchi kutokana na kuenea kwa vitendo vya ubadhirifu wa fedha miongoni mwa wabunge wa chama cha Liberal Democratic. Ishiba mara moja aliamuru ufanyike uchaguzi mdogo kwa matumaini ya kupata uungwaji mkono kwa kutumia ukosoaji wake, ili kuleta picha ya mageuzi.
Upigaji kura ulianza asubuhi kwa saa za huko leo Jumapili kote nchini Japan, ambapo wagombea 1,344, wakiwemo wanawake 314, wanawania nafasi ya uongozi.
Vituo vya kupigia kura vinafungwa saa mbili usiku kwa saa za huko, na matokeo ya awali yanatarajiwa kutolewa ndani ya saa chache.
Ishiba ameweka lengo la kushikilia viti 233 kwa muungano wa chama tawala kati ya LDP, na mshirika wake mdogo Komeita unaoungwa mkono na wa Budha, katika wingi wa viti kwa bunge la wawakilishi lenye wanachama 465, ambalo ndilo lenye nguvu zaidi katika bunge la Japan lenye viti viwili.