Waliohusishwa na rushwa Liberia watakiwa kujiuzulu

Chama kikuu cha upinzani cha Liberia, Congress for Democratic Party (CDC), kimewataka maafisa wote waliotuhumiwa kuhusika katika kashfa ya rushwa inayoendelea nchini humo kutoka kwenye nafasi zao wakati utaratibu wa kufunguliwa mashtaka ukiendelea.

Mulbah Murlue, Makamu Mwenyekiti wa operesheni na uhamasishaji katika chama cha CDC, anasema zaidi ya raia wa Liberia 300 wataanza mgomo wa chakula leo Jumatano ili kufikisha ujumbe wao.

Akizungumza na Sauti ya Amerika, Murlue amesema "asilimia 95 ya raia hao ni wanachama wa CDC ambao wanasema wamechoshwa na rushwa iliyoikithiri katika kila sekta ya Serikali. Wameamua kuchukua hatua mbadala katika kuokoa taifa na serikali ya kidemokrasia"