Idadi ya watu Burundi yaongezeka

Watoto nchini Burundi

Your browser doesn’t support HTML5

Idadi ya watu Burundi yaongezeka

Julai 11 ni siku ya kimataifa ya watu. Umoja wa matiafa ilitenga kuadhimisha siku hiyo tangu mwaka 1989.

Burundi inajiunga na mataifa mengine kuadhimisha siku ya kimataifa ya watu, kwa kuzingatia juu ya kasi kubwa ya ongezeko la watu katika taifa hilo linalokabiliwa na umasikini mkubwa, na ikiwa na changamoto kubwa za maendeleo endelevu.

Kwa wastani nchini Burundi, mzazi anajifunguwa watoto hadi sita. Wakazi wa taifa hilo wameongezeka takriban mara mbili zaidi katika kipindi cha miaka 30. Wataalam wanaishauri serikali kuchukuwa hatua za kulazimisha wazazi kutozidisha kuzaa watoto watatu kwa kila familia, ili kasi ya ongezeko la watu iweze kudhibitiwa.