Burundi yakanusha takwimu za UNHCR

Wakimbizi wa Burundi wanaokimbia ghasia za kisiasa nchini mwao na kwenda nchi jirani.

Serikali ya Burundi imekanusha vikali takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi - UNHCR kuwa ni wakimbizi Wakirundi zaidi ya 430,000 wanaohitaji misaada mwaka 2018.

Hayo yamejiri wakati shirika hilo limeanza kampeni ya kuchangisha pesa zaidi ya dola milioni 300 kwa ajili ya kuwahudumia wakimbizi hao ambao asilimia 80 wanaishi katika kambi za wakimbizi kwenye mataifa jirani.

Burundi inasema UNCHR imekuwa ikidanganya juu ya idadi ya wakimbizi kutoka nchini Burundi ili wajipatie kiwango kikubwa cha misaada kutoka kwa wafadhili.

Fuatilia taarifa ya mwandishi wetu wa Bujumbura, Haidallah Hakizimana.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Haidallah Hakizimana wa Burundi