Brexit : EU na Uingereza wakubaliana kuongeza muda wa mazungumzo

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen

Wajumbe kutoka Umoja wa Ulaya na Uingereza wameanza majadiliano katika juhudi mpya za kujaribu kufikia makubaliano ya kibiashara baada ya Uingereza kujiondoa katika umoja huo 2021.

Vyanzo vya habari vimeeleza kuwa hilo limefikiwa baada ya pande zote mbili kukubalina kuendelea na mazungumzo hayo.

Maafisa wa Uingereza wanasema utaratibu huo bado unamatumaini lakini Waziri Mkuu Boris Johnson ameonya kwamba matokeo huenda yakawa ni kutofikia makubalino.

Tarehe ya mwisho ya majadiliano ilikuwa jana jumapili lakini Johnson na Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen walikubaliana kuongeza muda.

Walizungumzia masuala ambayo hayakutanzuliwa na kusema yalikuwa ya manufaa na kuwataka wajumbe wao kuendelea na kuona Ikiwa watafikia makubaliano.

Tarehe ya mwisho ya Uingereza kujiondoa ni Disemba 31, na wasipokubaliana basi watatumia kanuni za Shirika la Biashara Duniani, WTO, katika kutoza kodi au ushuru wa bidhaa zao.