Biashara ya utumwa yashamiri Libya- Ripoti

Ramani ya Libya

Watu watano ambao walikuwa na hamasa ya kuongeza kipato chao, kupata uhuru wao na baadae kutelekezwa na kikundi cha kigaidi cha ISIS kama wafuasi wao, waliondoka Nairobi, Kenya na kupitia njia zinazojulikana za biashara yenye maslahi ya usafirishaji binadamu.

Wakiwa wameghilibiwa na vivutio vya udanganyifu ikiwemo kupata fedha na ajira, waliondoka Nairobi na kuelekea Busia kwa njia ya barabara. Baada ya hapo wakavuka mpaka wa Uganda.

Baadae waliendelea na safari yao hadi Kampala na kupenya huko katika mji wa Juba, ambapo Sudan Kusini inakabiliwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe, vyanzo vya habari nchini Kenya vimeripoti

Kituo chao cha pili kilikuwa Khartoum, Sudan na hatimaye wakawasili nchini Libya. Lakini, yale maisha waliokuwa wameahidiwa hayakupatikana.

Kwanza walikabiliwa na hali ngumu kutokana na joto kali na pia kuingizwa katika mafunzo magumu na kikundi cha kigaidi waliwaona hawafai, ambao ndiyo walikuwa waajiri wao.

“Walionekana kuwa hawana manufaa yoyote kwa kikundi hicho cha kigaidi na hatimaye waliwauza kama watumwa,” Taarifa za Kijasusi zimeripoti.

“Inaaminika kuwa kutokubaliana kati ya Wakenya hao na kikundi cha kigaidi ilikuwa siyo kwa sababu washiriki wao kutoka Kenya walikuwa hawawezi kukabiliana na hali ya hewa ya nchi hiyo, lakini ni pale walipotaka kujitoa katika kikundi hicho.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa :“Mtu anapojiunga na vikundi hivyo (vya kigaidi) huwezi kuondoka kwa hiari yako. Soko la utumwa nchini Libya limeelezwa kuwa kama ni shimo ambalo ukitumbukia huwezi kutoka, ambapo zama zimerejea katika siku za utumwa ambapo watu walikuwa wakiuzwa kwa wanunuzi wenye dau la juu."