Baraza la habari Kenya lasema halija kataza vyombo vya habari kuripoti matokeo

Watu wakiwa katika mstari kupiga kura katika uchaguzi mkuu 2022, Kenya

Mkuu wa baraza la habari la serekali ya Kenya anasema vyombo vya habari havijakatazwa kusimama kuhesabu matokeo ya kura za uchaguzi wa rais baada waangalizi kugundua kupungua kasi kuripoti uchaguzi huo wenye upinzani mkali.

Mkuu wa baraza la habari la Kenya, David Omwoyo, ameliambia shirika la habari la Associated Press Ijumaa kwamba hakuna chombo chochote kilicho zuiliwa kufanya hivyo, lakini akaongeza kusema kwamba wanataka kuwa na idadi sawa ya hesabu.

Anesena kwamba anakutana na viongozi wa vyombo vya habari wakati alipokuwa anaongea na AP.

Waangalizi na wanahabari pamoja na vyombo vya habari vya Kenya wameelezea wasiwasi wao bada ya kituo cha televisheni cha KTN, NTV Kenya, na Citizen TV ambavyo vinachukuwa matokeo kutoka mtando wa tume ya uchaguzi ambayo ilionekana kusimama ama kupunguza kasi kutoa matokeo siku ya Alhamisi.