Ban Ki-moon atembelea wakimbizi DRC.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- moon awasili Goma, DRC.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Jumanne alitembea mashariki mwa Congo ambako alikutana na wakimbizi katika eneo la Masisi.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Jumanne alitembea mashariki mwa Congo ambako alikutana na wakimbizi katika eneo la Masisi kwenye kijiji cha Kichanga kilomita 80 kaskazini magharibi mwa Mji wa Goma huko, Kivu kaskzini.

Your browser doesn’t support HTML5

Ban Ki-moon DRC.

Wakimbizi hao waliomba Umoja wa Mataifa uwasasidie kupata
Amani ili warudi kwenye vijiji vyao wakisema walikuwa wamechoshwa na maisha ya ukimbizi.

Katibu huyo amewaahidi kuwa atakutana na Rais Joseph Kabila ili serikali
ya Congo ishirikiane na kikosi cha Umoja wa Mataifa, MONUSCO katika kutokomeza makundi ya waasi yalioko mashariki mwa nchii hiyo.