Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini Somalia ametoa wito wa kuungwa mkono kimataifa wanajeshi wa serikali ya Somalia wanaopambana na kundi la wanamgambo wa Al Shabab katika nyanja mbalimbali nchini humo.
Mohamed El-Amine Souef, anasema jeshi la Somalia linahitaji siyo tu mafunzo bali pia silaha, vifaa, na ujuzi kwa maafisa wake, na kuondoa vikwazo vya silaha ili nchi iweze kununua silaha.
Katika mahojiano na VOA, Souef anasema Somalia ina jeshi changa na kuna wajibu kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia katika masuala si tu la nguvu kazi lakini pia silaha na risasi, na ujuzi.
“Mmeona kilichotokea Israel, katika mzozo wa Hamas na Israel, washirika wao ikiwa ni pamoja na Marekani, mara moja walichukua uamuzi wa kuiunga mkono Israel, kwa kutoa misaada ya kijeshi mara moja ndani ya siku kadhaa.