Mapema Jumatatu, Bw Gates alikuwa mjini Jerusalem ambako alizungumzia juu ya nia yampango wa nyuklia wa Iran na waziri mwenzake wa Israel, Ehud Barak. Bw Barak alisema, Israel haiondoi uwezekano wa hatua ya aina yeyote kuchukuliwa kuhusiana na mpango wa nyuklia wa Iran, lakini alisema kipaumbele kinabaki kuwa diplomasia. Bw Gates alikutana pia na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Wakati huo huo mjumbe maalum wa Marekani kwa ajili ya Mashariki ya Kati George Mitchell alikuwa huko Israel na kukutana na rais Shimon Peres siku ya Jumatatu. Hapo tena alisafiri hadi Ukingo wa Magharibi kwa mazungumzo na rais wa mamlaka ya Wapalestina Mahamoud Abbas, na mpatanishi mkuu wa Abbas, Saeb Erekat.
Kabla ya hapo asubuhi ya Jumatatu Bw. Mitchell alikutana na rais Hosni Mubarak wa Misri, mjini Cairo.