Aliyechukua nafasi ya pili, na hivyo kupata medali ya fedha ni Mkenya mwenzake, Brigid Kosgei, kwa kumaliza mbio hizo kwa saa 2, dakika 27 na sekunde 36.
Mmarekani Molly Seidel, alishika nafasi ya tatu kwa muda wa saa 2, dakika 27 na sekunde 46.
Waandaaji wa Olimpiki walianzisha mbio za marathon za wanawake saa kumi na mbili asubuhi kwa saa za Japan, saa moja mapema kuliko ilivyopangwa, katika juhudi za kuwakinga wanariadha na joto kali na unyevu.
Chechirchir asherehekea ushindi baada ya kukabidhiwa medali ya dhahabu.
Wanariadha kumi na tano kati ya 88 hawakumaliza mbio hizo, zilizofanyika katika mji wa pwani wa Sopporo, karibu kilomita 1,100, kaskazini mwa Tokyo.
Kosgei, anayeshikilia rekodi ya dunia, na bingwa mwingine Ruth Chepngetich, ambaye pia ni raia wa Kenya, walitarajiwa kushinda dhahabu leo Jumamosi, lakini Chepngetich alishindwa kumaliza mbiyo hizo. Jepchirchir alimpita Kosgei karibu na mwisho wa mbio hizo, katika kilomita ya arobaini.