Matukio muhimu Afrika Agosti 17 hadi 23

Waandamanaji wa upinzani wahudhuria mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Uhuru kusherehekea kuondolewa madarakani rais Ibrahim Boubacar Keita,  Bamako, Mali, Aug. 21, 2020.

Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan (C) akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Bamako, Mali Aug. 22, 2020, katika juhudi za kimataifa kudumisha tena utawala wa kiraia baada ya mapinduzi ya kijeshi. 

Wananchi wa Mali wajitokeza kwa wingi kuunga mkono mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondowa madarakari rais Ibrahim Boubacar Keita siku ya Jumanne. Maandamano yalifanyika Ijuma Aug. 21, 2020.

Ujumbe wa upatanishi wa ECOWAS wakutana na viongozi wa mapinduzi wa Mali

Mtu mzee kabisa duniani Fredie Blom, afariki akiwa na umri wa miaka 116, Ogusti 22 2020, nyumbani kwake Delft, karibu na Cape Town. Picha ina muonesha akisherehekea miaka yake 116 hapo Mei 8, 2020.

Serikali zinazo hasimiana Libya, zakubali kusitisha mapigano yaliyokua yakiendelea tangu kupinduliwa na kuuliwa kwa Muammar Ghadafi 2011. Picha za majengo yaliyoharibiwa mjini Sirte, Libya August 18, 2020.

Waandamanaji wakimbia mjini Nairobi baada ya polisi kuwafyetulia mabomu ya kutoa machozi walipokua wanaandamana kupinga ulaji rushwa pamoja na wizi wa vita vya msaada kupambana na janga la virusi vya Corona. maandamano yalifanyika kwenye bustani ya Uhuru Park Nairobi, Kenya, Aug. 21, 2020.

WHO imesema kuna watu 100 waloambukizwa katika muda wa siku 100 zilizopita na ugonjwa wa Ebola katika jimbo la Equateur, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kwenye pita many kazi wa afya mjini Bikoro jimbo la Equater akijitayarisha kuweka dawa mitaani dhidi ya virusi vya ebola, May 13, 2018, dwakati wa mlipuko wa mwezi Mei..

Wapiganaji wa kundi la NDC-R wanashiriki kenye gwarida wanaposalimisha silaha zao huko DRC

Timu ya wanawake walinzi wa mbuga za wanyama Kenya wapambana na majangiri na COVID-19

Familia za wapiganaji wa kundi la NDC-R wasubiri kurudishwa katika maisha ya kawaida DRC

Miongoni mwa matukio muhimu wanajeshi wapindua serikali ya rais Ibrahim Boubacar Keita nchini Mali.