Uganda Tanzania zakusudia kujenga bomba la mafuta

Your browser doesn’t support HTML5

Tanzania imeitaka Uganda kumaliza utata wa kodi katika mradi wa mafuta ili kuharakisha ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima Magharibi mwa Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania. Hayo yanakuja siku moja baada ya Kampuni ya Total kutangaza kujitoa katika ujenzi wa bomba hilo.