Wapinzani Cameroon wataka kumondoa rais Paul Biya

Watu wameketi katika kivuli karibu na bango la Rais wa Cameroon Paul Biya, kaskazini magharibi mwa Limbe, sehemu ya Kiingereza, Septemba 26, 2018, kabla ya uchaguzi wa rais wa 2018.

Kampeni zinaendelea nchini Cameroon kwa matayarisho ya uchaguzi wa urais Octoba 7, wanasiasa wawili wa upinzani wakiahidi kumuondoa rais Paul Biya madarakani.

Kampeni zinaendelea nchini Cameroon kwa matayarisho ya uchaguzi wa urais Octoba 7, wanasiasa wawili wa upinzani wakiahidi kumuondoa rais Paul Biya madarakani.

Maurice Kamto wa chama cha Cameroon Movement for the Renaissance of Cameroon, na Akere Muna, wanamshutumu rais Biya kwa ufisadi, kuanguka kwa uchumi, sekta ya kilimo, ukosefu wa ajira na ukosefu wa usalama.

Wagombea wote wanaahidi kurejesha hali ya utulivu na usalama kaskazini magharibi na kusini magharibi mwa Cameroon, maeneo yanayokabiliwa na mashambulizi dhidi ya watu wanaosungumza kiingereza.