Upinzani Tanzania wasitisha maandamano ya “UKUTA”

Freeman Mbowe kiongozi wa Chama kikuu cha Upinzani Tanzania Chadema

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema kimetangaza kusitisha maandamano yake yajulikanayo kama Ukuta yaliyopangwa kufanyika alhamisi ili kutoa fursa kwa viongozi wa dini kuanzisha majadiliano na Rais John Magufuli.

Your browser doesn’t support HTML5

Tanzania UKUTA

Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe amesema hatua hiyo imefikiwa kwa kuzingatia maslahi makubwa ya taifa hasa wito uliotolewa na viongozi wa dini waliotaka maandamano hayo yasitishwe ili kutoa fursa ya majadiliano na rais John Magufuli.

Mvutano wa maandamano hayo umepelekea kuwepo na rai kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wa zamani nchini humo kutaka kuwepo suluhu ya mezani.

Chama hicho kimetoa onyo iwapo hakutapatikana suluhu katika muda huo basi maandamano hayo ya Amani yatafanyika tena Oktoba mosi mwaka huu.