FDC nchini Uganda chatishia kufanya maandamano nchi nzima

Kiongozi wa chama cha upinzani cha FDC huko Uganda, Dr.Kizza Besigye.

Chama kikuu cha upinzani nchini Uganda-FDC kimeitisha maandamano makubwa ya wafuasi wake yanayolenga kuilazimu serikali kuitikia ukaguzi wa lazima wa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Februari mwaka huu.

FDC iliiandikia polisi maombi ya kutaka kuruhusiwa kuandamana inavyohitajika kisheria huku chama hicho kikitaka ulinzi wa polisi wakati wa mandamano hayo na kuonya kwamba iwapo polisi watawanyima kibali chama hicho kilisema itabidi kutumia nguvu.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Kennes Bwire wa kampala, Uganda