Kampeni za kuwania urais nchini Uganda zimeingia siku ya tatu hii leo.
Wagombea wa upinzani Dkt Kiiza Besigye wa chama cha “Forum for democratic change” na aliyekuwa waziri mkuu Amama Mbabazi wa vuguvugu la “Go foward,” wakiendelea kuvutia umati mkubwa wa watu katika mikutano yao.
Rais wa sasa wa Uganda, Yoweri Museveni
Rais wa sasa Yoweri Museveni naye ameimarisha kasi akihutubia mikutano minne kila siku kwa kutumia usafiri wa ndege aina ya helicopter.
Rais Museveni anadai kugundua njama za Dkt Besigye kutaka kufanya udanganyifu katika hesabu ya kura.
Your browser doesn’t support HTML5
Ripoti ya Mwandishi Kennes Bwire kuhusu kampeni za uchaguzi Uganda