Wamsumbiji wapiga kura katika uchaguzi mkuu wenye ushindani mkubwa
Wapiga kura wamesimama kwa utulivu katika mistari mirefu kusubiri zamu ya kupiga kura zao katika kituo cha kupiga kura cha Maputo, Msumbiji, Oct. 15, 2014.
Vyeti vya kupiga kura vya wagombea watatu wa kiti cha rais Msumbiji.
Wapiga waonesha vitambulisho vyao kabla ya kupiga kura katika kituo cha kupiga kura katika mji mkuu wa Maputo, Msumbiji, Oct. 15, 2014.
Mgombea kiti cha rais wa chama tawala cha Frelimo, Filipe Nyusi akipiga kura yake katika uchaguzi mkuu kwenye kituo cha kupiga kura mjini Maputo, Oct. 15, 2014.
Mpiga kura anajitayarisha kwenda kupiga kura yake katika kituo kimoja mjini Maputo mji mkuu wa Msumbiji, Oct. 15, 2014.
Rais wa Msumbiji anaeondoka madarakani Armando Guebuza (Kushoto)anapiga kura yake katika uchaguzi mkuu wa Oct. 15, 2014 mjini Maputo.
Daviz Simango, mgombea kiti cha rais wa chama kipya cha MDM, aanapiga kura yake katika mji wa kati wa Beira, Msumbiji 15 Out, 2014
Kidole cha mpiga kura kikipakwa wino usofutika kwa urahisi baada ya kupiga kura kuhakikisha hatopiga tena kura katika uchaguzi mkuu wa Oct. 15, 2014.
Afonso Dhlakama, kiongozi wa zamani wa waasi wa chama cha Renamo ambae sasa ndiye kiongozi wa upinzani, akionesha kidole chake baada ya kupiga kura katika uchaguzi wa tato kujaribu kuchaguliwa rais huko Msumbiji.
Mwanamke akimbeba mtoto wake mgongoni anapiga kura katika kituo cha kupiga kura mjini Moputo, Msumbiji, Oct. 15, 2014.
Wapiga kura wakisimama kwa utulivu katika kituo cha kupiga kura mjini Maputo siku ya uchaguzi mkuu Oct. 15, 2014.
Wafuasi wa mgombea kiti cha rais wa chama tawala cha FRELIMO Filipe Nyusi wakimshangiria wakati wa siku ya mwisho ya kampeni za uchaguzi siku ya Jumapili nje ya mji mkuu wa Maputo. Oct.12, 2014 on the outskirts of Maputo, Mozambique.
Daviz Simango, mgombea kiti cha rais wa chama kipya cha upinzani cha MDM akiwa mjini Massinga, katika jimbo la Inhambane wakati wa kampeni za uchaguzi.
Mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi wa mgombea kiti cha rais wa chama cha MDM Daviz Simango katika jimbo la Nyassa.
Kampeni za uchaguzi wa mgombea kiti wa chama tawala cha Frelimo, Filipe Nyusi katika jimbo la Zambezi
Kampeni za uchaguzi za chama cha upinzani cha Renamo huko Pemba Oktoba 2014.