Matukio baada ya uchaguzi wa DRC

Polisi wa kupambana na ghasia wa Congo akisimama karibu na matiri yanawaka moshi kwenye mtaa wa wafuasi wa Tshisekedi Matete mjini Kinshasa

Wafuasi wa kiongozi wa upinzani wa Congo Etienne Tshiusekedi wakiwatupia mawe polisi wa kupambana na ghasia nje ya makao makuu ya kiongozi wao mjini Kinshasa

Wafuasi wa rais Joseph Kabila wakisherehekea katika barabara ya Kinshasa baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa Disemba 9 2011

Wafuasi wa rais Joseph Kabila wa Coingo wakisherehekea ushindi wake baada ya kutangazwa na tume huru ya uchaguzi, Disemba 9 2011.

Mtu anaewaangalia polisi wa kupambana na ghasia katika mtaa wa Matete ngome ya kiongozi wa upinzani Tshisekedi mjini Kinshasa baada ya kuzuka ghasia kufuatia kutangazwa matokeo ya uchaguzi.

Wafuasi wa kiongozi wa upinzani wa Congo Etienne Tshisekedi wakiandamana mjini Brussels Ubelgiji kupinga matokeo ya uchaguzi.

Wafanayakazi wa uchaguzi walojitolea wakihesabu kura katika kituo cha kuhesabu kura cha Fikin mjini Kinshasa

Wafanyakazi wa tume ya uchaguzi wakijaribu hesabu mifuko na sanduku zilizojaa kura katika kituo cha Fikin kituo kikuu cha kuhesabu kura mjini Kinshasa.

Polisi wa kupambana na ghasia wa Congo wakipiga doria ngome ya upinzani ya Matete baada ya kuzuka ghasia kufuatia kutangazwa matokeo ya uchaguzi.

Wafuasi wa kiongozi wa upinzani Tshisekedi wanajikuta kati kati ya poiisi wa kupambana na ghasia wanaofyetua mabomu ya machozi na walinzi wa rais mjini Kinshasa

Sherehe, ghasia, na matatizo yaliyofuatia kutanagzwa matokeo ya uchaguzi wa DRC Disemba 2011