Kuapishwa kwa viongozi wa Tanzania

Rais J. Kikwete akiupungia mkono umati wa watu walohudhuria sherehe za kuapishwa kwake kwenye uwanja wa Uhuru

Jeshi la Tanzania linatoa heshima mbele ya rais J.Kikwete wakati wa sherehe za kuapishwa kwa mhula wa pili

Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride la jeshi la Taifa kabla ya kula kiapo

Wachezaji wa ngoma ya Lizombe ambayo asili yake ni mkoani Ruvuma wakitoa burudani kwenye sherehe za kuapishwa rais

Umati wa watu waloshuhudia kuapishwa kwa rais wa Tanzania kwenye uwanja wa Uhuru

Rais Jakaya Kikwete akila kiapo mbele ya mwanasheria mkuu Augustino Ramadhani kwenye uwanja wa Uhuru

Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba baada ya kuapishwa kwa mhula wa pili

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe na Rais Joseph Kabila wakati wa sherehe za kuapishwa kwa rais Kikwete kwenye uwanja wa Uhuru

Rais Joseph Kabila wa DRC akimpongeza rais Kikwete baada ya kula kiapo

Umati wa watu walohudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais Jakaya Kikwete kwa mhula wa pili

Jaji Frederick Werema akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kuteuliwa kua Mwanasheria Mkuu wa serikali

Rais J. Kikwete akimkabidhi miongozo ya kazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema huko Ikulu

Mgombea wa chama cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba akimpongeza rais Jakaya KIkwete alipotangazwa mshindi wa uchaguzi wa Oktoba 31 2010

Rais mpya wa Zanzibar Dk. Mohamed Shein, (kulia) akila kiapo mbele ya jaji Mkuu wa Zanzibar Hamid Mahamoud, (kushoto), wakati wa sherehe za kumapisha Amani Stadium Zanzibar

Rais anaeondoka madarakani Zanzibar Amani Karume akimpongeza rais mpya Dk. Mohamed Ali Shein

Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Dk Mohamed Shein muda mfupi baada ya kuapishwa Zanzibar

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mshindi wa pili wa uchaguzi wa rais Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad wakati wa shereha za kuapishwa Rais mpya wa Zanzibar

Kuapishwa kwa rais J.Kikwete na Dk. M. Shein wa Zanzibar