Ajali ya meli Zanzibar

Meli ya LCT Spice Islanders ikiwa gatini kabla ya safari

Wanajeshi wakiwasaidia walonusurika kutokana na ajali ya meli ya LCT Spice Islanders, Zanzibar

Rais wa Zanzibar, Dk Ali M. Shein na Makamu wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif wakiwa wenye huzuni wakati walifika eneo la ajali ya meli ya Spice Islander.

Polisi na waokozi wakibeba majeruhi wa meli ya Mv Spice Island katika ufukwe wa bahari ya Nunwi Unguja

Mamia ya watu walojazana kuanzia uwanja wa Maisasa hadi hospitali kuu wakisubiri kutambua maiti zao kutokana na ajali ya meli ya LCT Spice Islanders

Makamu wa pili wa Zanzibar Seif Ali Iddi akifuatana na naibu kadhi mkuu wa Zanzibar Khamis Haji Khamsi wakitoka ndani ya hema maalum iliyojengwa kuwapokea maiti katika uwanja wa Maisara

Madaktari,wauguzi na watu wakipokea maiti ya kwanza ilofikishwa katika kiwanja cha Maisara kutoka ajali ya meli ya Spice Islander

Mmoja kati ya abiria waliookolewa afikishwa ufukweni Nungwi

Rais Dk. Ali M. Shein akiongoza zoezi la uokoaji Nungwe baada ya ajali ya meli mapema asubuhi.

Rais Dk. Ali M Shein akiwafariji walonusurika

Kikao cha viongozi wa serikali ya Zanzibar wakiwa Pemba kwa lengo la kuweka mikakati ya kukabiliana na juhudi za kuwapokea wahanga wa ajali ya meli ya MV Spice Islanders

Mamia ya watu inahofiwa wamefariki dunia kufuatia kuzama kwa meli ya abiria - LCT Spice Islanders - katika bahari ya Hindi ikiwa safarini kutoka Unguja kwenda Pemba.