Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 02:41

Zoezi la kuhesabu kura laanza Tunisia


watu wameanza kuhesabu kura katika uchaguzi wa bunge Tunisia.
watu wameanza kuhesabu kura katika uchaguzi wa bunge Tunisia.

Maafisa wa uchaguzi nchini Tunisia wanaendelea kuhesabu kura leo baada ya kufanyika upigaji kura kuchagua bunge la kwanza tangu katiba ilipobadilishwa mwezi Januari mwaka huu.

Matokeo ya kwanza yanatarajiwa kuanza kutangazwa leo, na siku ya mwisho ni Alhamisi.

Kwa matokeo ya sasa chama cha kiislam chenye msimamo wa kati Isamist Ennahda na chama kisichokuwa na msimamo wowote cha Nidaa Tounes, vilitarajiwa kuongoza katika uchaguzi wa Jumapili.

Vyama 90 vinashindana katika uchaguzi huo, ikiwa ni juhudi za kidemokrasia toka kuondolewa madarakani Zine El Abidine Bin Ali aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo mwaka 2011.

Chama cha Ennahda kilikuwa kinaongoza katika uchaguzi wa kimapinduzi kwa mwaka huo, na kiongozi wake Rachid Ghannouchi ameuelezea uchaguzi wa Jumapili kama wa kihistoria.

XS
SM
MD
LG