Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 02:50

Maoni ya waislamu wa Marekani juu ya maisha na uhuru wao


Akbar Ahmed, profesa wa chuo kikuu cha American.
Akbar Ahmed, profesa wa chuo kikuu cha American.

Ziara ya Marekani na kundi la vijana yamulika hisia za waislamu juu ya jinsi wamarekani wenzao wanavyofahamu juu ya imani, maisha uhuru na haki zao.

Kuna takriban waislamu million 7 wanoishi Marekani hii leo, lakini licha ya idadi hiyo kubwa, ni wamarekani wachache kabisa wanaofahamu dini ya kislamu. Vichwa vya habari vimewapelea watu wengi kuambatanisha dini hiyo na ghasia, ukosefu wa kustahmiliana na ugaidi, na kusababisha mivutano baina ya waislamu na watu wa dini nyengine nchini humu.

Na hii ndio maana Professa wa chuo kikuu cha American University, na msomi wa kiislamu, Akbar Ahmed, aliamua kuongoza ujumbe wa vijana watafiti kufanya ziara kote Marekani, kupima hisia za jamii ya kiislamu. Matokeo yao yamechapishwa kwenye video na kitabu kiitwacho Journey into America: the challenge of Islam, yaani safari ndani ya Marekani, na changamoto za dini ya kiislam.

'Journey into America' chronicles the Muslim-American experience in the years since 9/11.
'Journey into America' chronicles the Muslim-American experience in the years since 9/11.

Katika kipindi cha mwaka mmoja, profesa Akbar Ahmed, na timu yake ya utafiti walizuru miji 75 ya Marekani, wakitembelea zaidi ya misikiti mia moja, shule za kiislamu na nyumba za waislamu. Ziarani, timu hiyo ilifanya takriban mahojiano elfu 2 na wamarekani waislamu, wakiwauliza kuelezea juu ya maisha yao hapa Marekani. Profesa Ahmed anasema hakuna shaka kuwa mashambulizi mabaya ya September 11, mwaka 2001, yalofanywa na kikundi kidogo tu cha waislamu, kumefanya maisha ya wamarekani waislamu kuwa magumu zaidi.

“Wamarekani waislamu kwa kawaida wanatazamwa mara nyingine kwa mashaka, mara nyingine kwa kutofahamiwa. Kuna utata fulani kuhusiana na dini ya kiislamu yenyewe, hili limesababisha kuwepo mwanya, mwanya ambao ulitokea baada ya mashambulizi ya September 11, mwaka 2001, na hata japo miaka mingi imepita, kwa bahati mbaya mwanya huo bado ungalipo.” Alisema Profesa Ahmed.

Kitabu cha profesa Ahmed, kinaeleza juu ya hamu ya maisha ambayo waislamu wengi wamarekani wanasema wangali wanakumbuka, zile siku kabla ya mashambulizi ya 911, wakati ambapo waliweza kufurahia uhuru unohakikishwa na sheria, kukiwa na utata mdogo sana miongoni mwa jamii hapa. Bw. Ahmed anasema, walieleza jinsi hali ilivyobadilika tangu mashambulizi ya mwaka 2001, na jinsi ilivyoathiri hata waislamu vijana mashuleni mwao.

“Tulisikia habari zinazo vunja moyo, moja hasa ni kuhusu kijana mmoja mwenye umri wa miaka 10 huko New York. Kijana huyo alituambia kuwa anapokwenda shule, hupigwa na wenziwe kwa sababu wanamuona kama gaidi. Na mamake alikwenda Pakistan, na aliuwawa huko akiwa ndani ya basi lililolipuliwa na kuni la kigaidi la Taliban. Kwa hivyo, yeye kwa njia fulani amekabiliwa na shinikizo kutoka pande zote, upande mmoja kutoka kwa wanaharakati wenye siasa kali, na upande wa pili kutoka kwa ubaguzi ambao waislamu wanakabiliwa nao hapa Marekani.” Alisema Profesa Ahmed.

Licha ya ubaguzi, Bw. Ahmed anasema, waislamu hapa Marekani, bado wanakwenda mbio kusakaa ndoto ya kufanikiwa Marekani, yaani kwa lugha ya kimombo, American Dreams. Na wengi wananawiri katika nyanja kama vile, afya, sayansi, biashara, na hata ubunge. Kufaulu kwao, Ahmed anasema, kunaleta changa moto mpya. Nazo ni: kufanya kazi zaidi kuwaelimisha watu wa dini nyenginezo kuhusu uislamu, na kujibu kile ambacho waislamu wengi wanaamini ni mtazamo usiyo sahihi kuhusu uislamu, kwenye vyombo vya habari vya Marekani. Ahmed anasema hii ni katika juhudi zao kuziba mwanya huu wa kutokufahamiana, waislamu wamarekani nao pia wanahisia za dhati za uzalendo.

“Tukizungumzia waanzilishi wa taifa hili, kwa kuzungumzia viongozi kama vile George Washington, Thomas Jefferson, Benjamin Franklin na John Adams, wote waliwasiliana na watu wenye imani, kutoka dini yeyote duniani, na hata Uislam.” Alisema Profesa Ahmed.

Ahmed anasema dini ya kislamu inakabiliwa na changamoto pia kwa sababu pale wamarekani wanapotazama jamii za waislamu walowengi kote duniani, huwa wanaona zaidi, utawala wa kifalme, au utawala wa kidikteta, kuenea kwa dhulma, na ukosefu wa heshima kwa haki za kibindam. Mandhari hiyo mbaya inabuni fikra mbaya dhidi ya dini ya kiislamu hapa Marekani. Na fikra hizo zinaendelezwa, Ahmed anasema, kila mara kunapotokea kitendo cha uhalifu kinachofanywa na mtu kwa jina la Uislamu, kama vile mauwaji yalofanywa na Meja Nidal Malik Hassan, muislamu ambaye alikuwa daktari wa akili kwenye kambi ya Fort Hood huko Texas.

Karibu na mwisho wa kitabu chake, professa Ahmed anapendekeza, njia moja ambapo fikra hizo zinaweza kushindwa. Ikiwa Wamarekani waislamu na wasio waislamu, wanaweza kufikia lengo la pamoja, kwa manufaa yao wote, katika kusongeza mbele Marekani kuelekea kuwa na uhusiano bora na ulimwengu wa kiislamu. Kufanya hivyo, Ahmed anasema, serikali ya Marekani kwanza inahitaji kuendeleza uhusiano bora zaidi na raia wake waislamu.

“Maafisa wa serikali ya Marekani lazima wawe na uhusiano bora zaidi wa kufanya kazi na waislamu, kwa sababu waislamu ni jamii muhimu sana ya wachache hapa Marekani. Kuna takriban waislamu million 7, na ni jamii ambayo huwezi kuidharau. Wamarekani wanahitaji kufahamu na kuanza kwa dhati kuelewa hisia za jamii ya waislamu hapa Marekani kwa sabau Marekani iko katika mzozo hivi sasa katika jukwa la kimataifa huko Iraq, Afghanistan na Pakistan, na waislamu wanaweza kuwa na jukumu muhimu kama wajumbe baina ya wamarekani na dunia ya kiislamu.” Alisema Profesa Ahmed.

Akbar Ahmed anasema, anatumai kitabu chake kiitwacho Journey into America: The Challenge of Islam, kitawahimiza wamarekani kutoka kila nyanja kuwachukulia raia wenziwao waislamu kwa mtazamo mpya wa matumaini, na kutambua pengine kwa mara ya kwanza, kuwa waislamu ni kiungo muhimu cha jumuiya ya kimarekani.

XS
SM
MD
LG