Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 09:36

Zaidi ya wafungwa dazeni tatu wa Kipalestina warejea nyumbani

Rawda Abu Ajamieh akiwakumbatia jamaa na marafiki baada ya kuachiliwa kutoka jela ya Israel kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas katika kambi ya wakimbizi ya al-Duheishe katika Ukingo wa Magharibi wa Bethlehem, Novemba 24, 2023.

Zaidi ya wafungwa dazeni tatu wa Kipalestina wamerejea nyumbani wakipokelewa kishujaa huko  Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa kimabavu baada ya kuachiliwa kutoka kwente magereza ya Israel kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas.

Msafara wa wafungwa walioachiliwa, wengine wakituhumiwa kwa makosa madogo na wengine waliohukumiwa katika mashambulizi, ulichochea umati mkubwa wa Wapalestina kuimba, kupiga makofi, kupunga mikono, na kuwa na shamrashamra.

Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na watawala wa Gaza, Hamas yanahusisha kubadilishana, kwa muda wa siku nne, watoto na wanawake 150 wa Kipalestina waliokuwa katika jela ya Israel kwa mateka 50 wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas.

Wapalestina wengi wanaotarajiwa kuachiliwa siku zijazo ni vijana waliokamatwa kwa uchochezi na kurusha mawe.

Forum

XS
SM
MD
LG