Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 17:39

Zaidi ya nyumba 500 zahofiwa kuharibiwa na moto Colorado0


Anthony D-Amario, mkiaka 18, akiangalia kwenye mabaki ya nyumba yake iliyoharibiwa na moto huko Louisville, Colorado, Dec. 31, 2021.

Mamia ya wakazi wa Colorado  ambao walitarajia kuukaribisha  mwaka wa 2022 wakiwa majumbani mwao badala yake walijikuta wakiuanza mwaka mpya wakijaribu kuokoa kilichobaki kwenye nyumba zao baada ya upepo mkali sana uliosababisha moto kukumba viunga vya Denver.

Mamia ya wakazi wa Colorado ambao walitarajia kuukaribisha mwaka wa 2022 wakiwa majumbani mwao badala yake walijikuta wakiuanza mwaka mpya wakijaribu kuokoa kilichobaki kwenye nyumba zao baada ya upepo mkali sana uliosababisha moto kukumba viunga vya Denver.

Familia zililazimika kuukimbia moto huku kukiwa na onyo dogo la kurejea kwenye ujirani wao siku ya Ijumaa na kukukaribishwa na uharibifu mkubwa. Baadhi ya maeneo na nyumba ziliungua kabisa na moto zikiwa karibu na nyingine ambazo hazikuguswa na moto.

“Kwa miaka 35 nilitembea nje ya mlango wa nyumba yangu, niliziona nyumba nzuri,” Eric House alisema. “Ninapotembea nje, nyumba yangu ilipokuwa. Natembea nje ya mlango wa mbele na hiki ndiyo ninachokiona.”

Watu saba walijeruhiwa, lakini cha kutia moyo ni kwamba hakuna ripoti zozote za vifo au mtu yeyote aliyepotea katika moto wa msituni ambao ulizuka Alhamisi ndani na kuzunguka Louisville na Superior, miji jirani kiasi cha kilometa 32 kaskazini magharibi mwa Denver huku kukiwa na mchanganyiko watu 34,000.

Zaidi ya nyumba 500 zilikhofiwa kuharibiwa, na hivi sasa wamiliki wa nyumba wanakabiliwa na jukumu zito ya kujenga tena huku kukiwa na uhaba wa bidhaa ambao umetokana na janga la miaka miwili.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG