Hilo limefanyika mwezi mmoja baada ya makubaliano ya kisitisha mapigano ikiwa kama juhudi ya kumaliza ghasia za miaka miwili kwenye jimbo la Tigray kaskazini mwa nchi.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kamanda huyo Tadesse Wereda amesema kwamba asilimia 65 ya wapiganaji wake wameweka silaha chini, kupitia video kwenye ukurasa rasmi wa TPLF mwishoni mwa wiki.
Msemaji wa serikali ya Ethiopia Legesse Tulu hajasema lolote hata baada ya kuulizwa kufanya hivyo. Vita vilizuka nchini humo Novemba 2020 kati ya vikosi vya TPLF na jeshi la serikali pamoja na washirika wake vikiwemo vikosi vya jimbo jirani la Tigary la Amhara, pamoja na vikosi vya nchini jirani ya Eritrea.
Facebook Forum