Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 15:59

Zaidi ya 64 wafa katika mkanyagano India


Maiti zilizotapakaa nje ya Hekalu ya Kihindu baada ya mkanyagano Octoba 13, 2013
Maiti zilizotapakaa nje ya Hekalu ya Kihindu baada ya mkanyagano Octoba 13, 2013
Maafisa wa India wanasema zaidi ya watu 64 wameuawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa katika mkanyagano kwenye daraja nje ya hekalu ya kihindu katika jimbo la Madhya Pradesh, huku wengi wakiruka daraja hilo na kutumbukia mtoni.

Jumapili, polisi huko India walionya kuwa idadi ya vifo inaendelea kuongezeka huku maafisa wa afya wakijitahidi kuwafikia waliojeruhiwa kwa wakati, baada ya uvumi kuwa daraja hilo lililikuwa linakaribia kuanguka.

Aidha maafisa hao wanasema mkanyagano huo ulianza kwenye kivuko cha daraja la mto Sindh wakati umati wa watu ulipokuwa unavuka daraja hilo kuhudhuria sherehe za kidini.

India ina historia ndefu ya maafa ya mkanyagano wakati wa sherehe za kidini.
XS
SM
MD
LG