Aprili 24 hadi Aprili 30 ni Wiki ya Chanjo Duniani, ambapo Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu 2023 ni The Big Catch-Up.
Lengo ni kwa kila mtu, hasa watoto, kupata chanjo ambazo huenda walizikosa wakati wa mlipuko wa virusi vya corona.
Lengo kuu la Wiki ya Chanjo Duniani kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO) ni watoto zaidi, watu wazima na jamii zao kulindwa dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo kama vile polio na surua.