Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Agosti 25, 2026 Local time: 13:20

WHO yadai kupiga hatua katika kukabiliana na kesi za manyanyaso ya ngono miongoni mwa wafanyakazi

Picha ya maktaba inayoonyesha jina la WHO
Picha ya maktaba inayoonyesha jina la WHO

Shirika la Afya Duniani WHO limesema mapema wiki hii kwamba limepiga hatua katika kukabiliana na kesi za manyanyaso ya ngono, ingawa bado ni tatizo kubwa miongoni mwa wafanyakazi wake.

“Katika miaka miwili iliyopita, WHO imejitahidi kuzuia na kushugulikia aina yoyote ya utovu wa nidhamu unaohusisha masuala ya ngono, manyanyaso ya ngono", amesema Gaya Gamhewage, mratibu wa kuzuia na kushughulikia tatizo hilo kwenye WHO.

Amesema hata hivyo kwamba idadi ya kesi zinaendelea kuongezeka, lakini hilo halina maana kwamba juhudi zao hazisaidii. Ameongeza kusema kwamba juhudi zao zimeendelea kufichua kesi zaidi. Ndani ya kipindi cha miezi 12 iliyopita, ofisi ya uangalizi wa ndani ya WHO, imesema kwamba imechunguza kesi 287 za manyanyaso ya ngono kutoka matawi yote ya WHO.

Gamhewage amesema kwamba kesi hizo zinahusishwa wafanyakazi, wanakandarasi, pamoja na washirika, na wala siyo walinda usalama.

Forum

XS
SM
MD
LG