Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:46

WHO imetoa tahadhari dhidi ya dawa za kifua kwa watoto


Nembo ya shirika la afya duniani (WHO) mjini Geneva
Nembo ya shirika la afya duniani (WHO) mjini Geneva

Tahadhari hiyo iliyotolewa Jumatano inakuja baada ya mamlaka ya Uzbekistan kusema mwezi uliopita takriban watoto 20 walifariki baada ya kutumia dawa hiyo ya kunywa na siyo kidonge iliyotengenezwa na kampuni kwa jina Doc-1 Max

Shirika la afya duniani (WHO) limetoa tahadhari dhidi ya matumizi ya dawa mbili za ugonjwa wa kukohoa za India zinazolalamikiwa kusababisha vifo vya watoto wasiopungua 20 nchini Uzbekistan.

WHO imesema bidhaa hizo zilizotengenezwa na kampuni ya Marion Biotech ya India, zilikuwa "chini ya viwango" na kwamba kampuni hiyo imeshindwa kutoa uhakikisho kuhusu "usalama na ubora wake".

Tahadhari hiyo iliyotolewa Jumatano, inakuja baada ya mamlaka ya Uzbekistan kusema mwezi uliopita takriban watoto 20 walifariki baada ya kutumia dawa hiyo ya kunywa na siyo kidonge iliyotengenezwa na kampuni kwa jina Doc-1 Max.

Wizara ya afya ya India baadaye ilisitisha uzalishaji katika kampuni hiyo na Uzbekistan ilipiga marufuku uagizaji na uuzaji wa Doc-1 Max.

XS
SM
MD
LG