Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 19:04

Wazee waachiliwa huru na Islamic State


Kundi la ufuatiliaji haki za biunadamu nchini Syria, linasema wakristu wa Syria ambao ni wazee waliokuwa wameshikiliwa na Islamic State wameachiliwa.

Kundi lenye makao yake uingereza la Syrian Observatory for Human Rights, lenye mtandao nchini humo linaripoti kwamba baadhi ya wakazi waliotekwa Tal Koran waliachiwa Jumapili.

Wanamgambo wa Syria walisema karibu watu 150 walichukuliwa na Islamic State baada ya vijiji vyao kushambuliwa karibu na mto Khabour kaskazini mashariki mwa Syria.

Wiki iliyopita, Islamic State walivamia miji kadhaa yenye wakristo wengi.

Wakati huohuo, vikosi vya waasi huko Aleppo vimekataa mpango wa Umoja wa Mataifa wa amani kumaliza kadhia ndani ya Syria.

Waasi wamesema hawatojiondoa katika juhudi za kupambana na kadhia ya watu wanaolengwa na silaha za kikemikali za utawala na kutumika kwa mabomu yaliyo katazwa na jumuiya ya kimataifa.

XS
SM
MD
LG