Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 14:59

Watu zaidi ya 90 wauwawa katika ajali Sierra Leone


Tukio la ajali linaonekana baada ya lori la mafuta kulipuka huko Freetown, Sierra Leone Novemba 6, 2021 .

Takriban watu 91 wameuawa katika mji mkuu wa Sierra Leone siku ya Ijumaa wakati lori la mafuta lilipolipuka kufuatia ajali.

Takriban watu 91 wameuawa katika mji mkuu wa Sierra Leone siku ya Ijumaa wakati lori la mafuta lilipolipuka kufuatia ajali, chumba cha kuhifadhi maiti na maafisa wa eneo hilo wamesema.

Serikali bado haijathibitisha idadi ya waliofariki, lakini meneja wa chumba cha kuhifadhi maiti mjini Freetown alisema wamepokea miili 91 kufuatia mlipuko huo.

Waathirika ni pamoja na watu ambao walikuwa wamemiminika kuchota mafuta yaliyokuwa yanavuja kutoka kwenye tenka lililopasuka, Yvonne Aki-Sawyerr, meya wa mji wa bandari, aliandika kwenye ukurasa wa Facebook.

Tuna majeruhi wengi, na maiti zilizoungua," alisema Brima Bureh Sesay, mkuu wa Shirika la Kitaifa la Kudhibiti Maafa, kwenye video kutoka eneo la tukio iliyosambazwa mitandaoni. "Ni ajali mbaya sana” alisema.

Picha zilizosambaa sana mtandaoni zilionyesha waathirika kadhaa walioungua vibaya wakiwa wamelala barabarani huku moto ukiwaka kwenye maduka na nyumba zilizo karibu. Reuters haikuweza kuthibitisha picha hizo mara moja.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG