Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 18:51

Watu 19,000 wamehamishwa majumbani mwao kutokana na mioto ya msituni Ugiriki


Miongoni mwa wakaazi wa kisiwa cha Rhodes nchini Ugiriki wakiondoka kwenye eneo kutokana na moto unaowaka. July 22, 2023.
Miongoni mwa wakaazi wa kisiwa cha Rhodes nchini Ugiriki wakiondoka kwenye eneo kutokana na moto unaowaka. July 22, 2023.

Polisi wa eneo hilo nchini Ugiriki walisema watu 16,000 walihamishwa kwa njia ya barabara na 3,000 kwa njia ya bahari kutoka vijiji 12 na hoteli kadhaa, hakuna vifo vyovyote vilivyotokea hadi wakati huu

Takriban watu 19,000 wamehamishwa kutoka kisiwa cha Rhodes nchini Ugiriki wakati mioto ya msituni ikiendelea kuwaka kwa siku ya sita katika maeneo matatu, mamlaka ya Ugiriki imesema Jumapili.

Wizara ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Ulinzi wa Raia imesema kuwa ni uhamishaji mkubwa zaidi kutokana na moto wa msituni nchini humo. Polisi wa eneo hilo walisema watu 16,000 walihamishwa kwa njia ya barabara na 3,000 kwa njia ya bahari kutoka vijiji 12 na hoteli kadhaa, hakuna vifo vyovyote vilivyotokea hadi wakati huu.

Watu sita walilazwa hospitali kwa muda mfupi wakiwa na matatizo ya kupumua na baadaye wakaruhusiwa. Jumapili asubuhi kwa saa za huko, wafanyakazi wa zima moto 266 na magari 49 katika eneo waliungana na helikopta tano na ndege 10, ambapo saba za Ugiriki, mbili za Uturuki na moja ya Croatia kuwasaidia kuzima moto huo, mamlaka imesema.

Magari mengine 15 yanatarajiwa baadaye hii leo.

Forum

XS
SM
MD
LG