Watu 15 wengi wao raia, waliuawa katika mashambulizi sambamba mwishoni mwa wiki huko mashariki mwa Burkina Faso, vyanzo vya usalama na vya kieneo vimeliambia shirika la habari la AFP leo Jumanne.
Nchi hiyo ya Afrika Magharibi inapambana na uasi wa wanajihadi ambao ulisambaa kutoka nchi jirani ya Mali mwaka 2015 na kusababisha vifo vya zaidi ya raia 17,000 wakiwemo pia wanajeshi na kuwakosesha makazi watu milioni mbili.
Katika ghasia za hivi karibuni watu 15 wakiwemo wasaidizi watatu wa jeshi waliuawa Jumamosi katika mashambulizi huko Diapaga, mji mkuu wa mkoa wa Tapoa upande wa mashariki, mkazi wa eneo hilo ameliambia shirika la habari la AFP.
Kondia Pierre Yonli, msemaji wa shirika la kiraia la mkoa huo alithibitisha taarifa hizo akiongeza kuwa shule, masoko, na huduma za umma zilisimamishwa katika mkoa huo leo Jumanne kwa ajili ya kuwapa heshima waathirika ambao walizikwa Jumapili katika makaburi ya manispaa ya Diapaga.
Forum