Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 05:15

Watu 10 wameuwa katika shambulizi la risasi California nchini Marekani


Polisi katika eneo la tukio la ufyatuaji risasi kwenye mji wa Monterey Park huko Los Angeles, California

Ufyatuaji risasi ulifanyika baada ya saa nne usiku kwa saa za huko karibu na mahala panakofanyika sherehe za Mwaka Mpya wa China zilizofanyika Monterey Park vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti. Monterey Park ni mji ulio karibu kilomita 11 kutoka katikati ya jiji la Los Angeles.

Watu 10 waliuawa katika shambulizi la risasi katika mji wa Monterey Park, kwenye jimbo la California katika ukumbi wa dansi Jumamosi usiku, Idara ya Polisi ya Kaunti ya Los Angeles nchini Marekani imesema.

Mshukiwa aliyekuwa na silaha alitoroka kwenye eneo la tukio na polisi bado wanajaribu kumtafuta, idara hiyo ilisema mapema Jumapili.

Bado hakuna taarifa kuhusu sababu ya shambulizi hilo, idara hiyo iliongeza.

Watu wengine 10 walipelekwa katika hospitali za eneo hilo kutibiwa majeraha na angalau mtu mmoja alikuwa mahututi

Ufyatuaji wa risasi ulifanyika baada ya saa nne usiku kwa saa za huko karibu na mahala panakofanyika sherehe za Mwaka Mpya wa China zilizofanyika Monterey Park, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti. Monterey Park ni mji ulio karibu kilomita 11 kutoka katikati ya jiji la Los Angeles.

Picha za video zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha watu waliojeruhiwa wamebebwa kwenye machela wakipelekwa kwenye magari ya kubeba wagonjwa wakiwa na wahudumu wa huduma za dharura. Kuzunguka eneo la tukio la ufyatuaji risasi polisi walifunga mitaa kwa utepe wa njano video hiyo ilionyesha.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG