Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 19:47

Watatu wauwawa kwa makombora ya  Russia katika mji wa Odesa


Sehemu ya kituo cha biashara imeharibiwa baada ya shambulio la usiku la roketi la Russia huko Odesa, Ukraine, Jumatano, Juni 14, 2023.(AP).
Sehemu ya kituo cha biashara imeharibiwa baada ya shambulio la usiku la roketi la Russia huko Odesa, Ukraine, Jumatano, Juni 14, 2023.(AP).

Makombora ya  Russia yamefyetuliwa hadi mji wa bandari wa Odesa Kusini mwa Ukraine mapema Jumatano, na kuua takriban watu watatu na wengine 13 kujeruhiwa.

Jeshi la Ukraine limesema kwamba makombora yaliyotumiwa katika shambulio hilo ni manne ya kwenda masafa vya mbali yaliyopewa jina la Kalibr.

Maafisa wa jimbo wamesema kuwa makombora yalipiga ghala ambapo watu hao watatu waliuawa na kwamba shambulio la Russia pia liliharibu nyumba na maduka katikati mwa jiji la Odesa.

Maafisa walisema waokoaji walikuwa wakitafuta mtu yeyote ambaye huenda alikuwa amezikwa kwenye vifusi.

Forum

XS
SM
MD
LG