Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 22, 2024 Local time: 11:13

Watanzania wasubiri matokeo ya ucgauzi

Wapiga kura wakiwa kwenye zoezi la kupiga kura Jumapili Oktoba 25,2015
Wapiga kura wakiwa kwenye zoezi la kupiga kura Jumapili Oktoba 25,2015

Chama tawala cha CCM kinapata shinikizo kubwa kusukuma mbele maendeleo na kukabiliana na ongezeko la kiwango kikubwa cha umasikini.

Maafisa wa uchaguzi nchini Tanzania wanasema wanatarajia kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi Jumatatu baada ya upigaji kura wa Rais na wabunge kufanyika Jumapili.

Chama tawala cha CCM kinapata shinikizo kubwa kusukuma mbele maendeleo na kukabiliana na ongezeko la kiwango kikubwa cha umasikini.

Chama kicho kilipata changamoto katika vituo vya kupigia kura kutoka muungano wa vyama vya upinzani – UKAWA ambavyo vilimteuwa aliyekuwa waziri mkuu wan chi hiyo Edward Lowassa kama mgombea wake.

Jumapili Lowassa alipiga kura yake aliwashawishi wengine kufanya kama yeye.

Alisema ipo amani nchini Tanzania, isipokuwa wote wanatakiwa kutoka nje na kupiga kura kwa sababu hiyo ndiyo fursa pekee ili kubadilisha historia ya nchi hiyo.

Maafisa wa tume ya buchaguzi wameeleza kujiamini kwao kufuatia zoezi la upigaji kura ambalo litaamuliwa kwa haki na usawa licha ya kuripotiwa kuwa na kasoro katika baadhi ya vituo vya kupigia kura.

XS
SM
MD
LG