Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 05, 2022 Local time: 21:23

Wasichana watatu wa Uingereza waonekana katika video Uturuki


A combination of handout CCTV pictures received from the Metropolitan Police Service shows (L-R) British teenagers Kadiza Sultana, Amira Abase and Shamima Begum passing through security barriers at Gatwick Airport, south of London, on Feb. 17, 2015.

Wasichana watatu wa Kiingereza ambao inasadikika wamesafiri nchini Syria kujiunga na kundi la kigaidi la Islamic State, wameonekana katika picha za video za usalama za Uturuki.

Vyombo vya habari vya Uturuki vimesema picha zinawaonyesha wasichana hao wadogo wakipanda basi mjini Instanbul.

Ni picha za kwanza kuripotiwa za wasichana hao toka walipoondoka London, karibu wiki mbili zilizopita.

Maafisa wa usalama wamesema hawana sababu ya kuamini kwamba wasichana hao bado wapo nchini Uturuki na wanaamini wamevuka mpaka kuingia nchi ya jirani ya Syria ambayo sehemu yake imechukuliwa na kundi la kigaidi la Islamic State.

Wasichana hao watatu waliokuwa wanasoma darasa moja mashariki mwa Londan, Shamima Begum miaka 15, Kadiza Sultana miaka 16, na Amira Abase miaka 15, walipanda ndege ya shirika la Uturuki kutoka London kwenda Instanbul Febuari 17.

XS
SM
MD
LG