Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 11:03

Wapalestina wachukua hifadhi kwenye shule na hospitali huko Gaza


Watu wakiondoka makwao kutokana na mapigano huko Gaza.
Watu wakiondoka makwao kutokana na mapigano huko Gaza.

Wapalestina waliozingirwa huko Gaza Jumatatu wamekusanyika kwenye hospitali na shule wakitafuta hifadhi, huku chakula na maji vikipungua. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, zaidi ya watu milioni moja wamekimbia makazi yao kabla ya  mashambulizi ya ardhnii ya Israel.

Wakati bidhaa kama chakula, maji na dawa zikiendelea kupungua, matumaini yapo kwenye kivuko cha mpakani cha Rafah kati ya Gaza na Msiri, ambako malori yaliyobeba misaada yamekuwa yakisubiri wapatanishi kushinikiza sitisho la mapigano ambalo litawaruhusu wao kuingia Gaza, na kuwaruhusu wageni kuondoka.

Wizara ya afya ya Gaza imesema wapalestina 2,750 wameuwawa huku wengine 9,700 wamejeruhiwa tangu mapigano yalipozuka, ikiwa idadi kubwa kuliko ile ya vita vya Gaza vya 2014 vilivyodumu kwa zaidi wiki 6.

Zaidi ya wa Israeli 1,400 wamekufa, wengi wakiwa raia waliouwawa kwenye shambulizi la Hamas la Oktoba 7. Jeshi la Israel limesema Jumatatu kwamba takriban mateka 199 walipelekwa Gaza wakati wa shambulizi hilo, ikiwa idadi kubwa kuliko makadirio ya awali. Hata hivyo haijabainishwa iwapo kuna raia wa kigeni miongoni mwao.

Forum

XS
SM
MD
LG