Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 15:46

Wanajeshi wanane wamekufa Burkina Faso katika shambulizi la kushtukiza


Ramani ya Burkina Faso na nchi jirani
Ramani ya Burkina Faso na nchi jirani

Shambulizi hilo lilitokea Ijumaa katika Deou na Oursi katika jimbo la Oudalan ilisema taarifa hiyo. Wanajeshi wanane waliuawa, watatu walijeruhiwa na wengine kadhaa hawajulikani walipo ilisema taarifa ikielezea idadi hiyo

Wanajeshi wanane wamekufa katika shambulizi la kushtukiza linaloshukiwa kufanywa na wanajihadi huko kaskazini mwa Burkina Faso jeshi lilisema Jumatatu likiongeza kwamba takribani washambuliaji 60 waliuawa katika shambulizi la kujibizana.

Shambulizi hilo lilitokea Ijumaa katika Deou na Oursi katika jimbo la Oudalan ilisema taarifa hiyo. Wanajeshi wanane waliuawa, watatu walijeruhiwa na wengine kadhaa hawajulikani walipo ilisema taarifa ikielezea idadi hiyo.

Kiasi cha magaidi 60 waliuawa katika shambulizi la angani la kujibizana lililolenga maeneo ya adui ambayo walijaribu kukimbia kuelekea mpakani huko kaskazini kuelekea Mali, ilisema taarifa. Magari saba ya kijeshi na darzeni za pikipiki pia ziliharibiwa. Taarifa ilitoa wito dhidi ya kutangaza idadi isiyo rasmi hadi vifo vitakapothibitishwa kwenye eneo.

XS
SM
MD
LG