Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 03:27

Wanajeshi 13 wa Burkina Faso wameuawa na wanajihadi wa nchini humo


Wanajeshi wa Burkina Faso wameuawa na washukiwa wanajihadi (Hii ni picha ikielezea vifo vya wanajeshi Burkina Faso siku za nyuma vikihusishwa na wanajihadi mjini Ouagadougou, Oct. 8, 2022)
Wanajeshi wa Burkina Faso wameuawa na washukiwa wanajihadi (Hii ni picha ikielezea vifo vya wanajeshi Burkina Faso siku za nyuma vikihusishwa na wanajihadi mjini Ouagadougou, Oct. 8, 2022)

Wanajeshi wanne wa jeshi la  ulinzi pia walijeruhiwa katika shambulio la Jumamosi kwenye barabara inayounganisha Fada N'Gourma na Natiaboani, moja ya vyanzo hivyo vimesema

Washukiwa wanajihadi wamewavamia na kuwaua wanajeshi 13 katika jimbo la mashariki nchini Burkina Faso, vyanzo vya usalama vimeliambia shirika la habari la AFP jumapili katika ghasia za hivi karibuni kulitikisa taifa hilo la Afrika Magharibi lililokumbwa na uasi.

Wanajeshi wanne wa jeshi la ulinzi pia walijeruhiwa katika shambulio la Jumamosi kwenye barabara inayounganisha Fada N'Gourma na Natiaboani, moja ya vyanzo hivyo vimesema.

"Vikosi vimetumwa kulinda eneo hilo na kufanya upekuzi," chanzo cha pili kiliongeza, kikithibitisha idadi ya vifo. Kikosi kilichovamiwa kilikuwa kimetumwa kuchukua nafasi ya kikosi kingine kutoka Natiaboani.

Uvamizi huo unakuja baada ya kundi lenye nguvu la Support Group for Islam and Muslim (GSIM), ambalo lina uhusiano na al-Qaeda, kudai Ijumaa lilitekeleza shambulizi dhidi ya kambi ya kijeshi huko Djibo, mji mkubwa wa kaskazini ambao umekuwa chini ya vizuizi vya wanajihadi kwa miezi mitatu.

Jeshi limesema takriban wanajeshi 10 walifariki na wengine 50 kujeruhiwa katika shambulio hilo la "kigaidi" katika kikosi cha 14 siku ya Jumatatu.

XS
SM
MD
LG