Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 21:21

Wamarekani kuanza kusafiri Cuba bila Masharti


Bendera ya Cuba kushoto na Marekani kulia.
Bendera ya Cuba kushoto na Marekani kulia.

Wizara ya fedha ya Marekani inasema taratibu mpya za kulegeza masharti ya biashara na usafiri kwenda na kutoka nchini Cuba, zitatekelezwa kuanzia Ijumaa.

Hatua hiyo ni muendelezo wa lengo la uongozi wa Rais Barack Obama, alilotangaza mwezi Desemba 17 mwaka jana.

Bwana Obama alitangaza kuanza kuwepo kwa uhusiano wa kawaida na nchi ya Cuba ambayo ni nchi ya kikomunisti.

Katika utaratibu huo mpya, Wamarekani hawatahitaji kuomba vibali ili kusafiri kwenda Cuba, kwa sababu yoyote ile kati ya darzeni ya sababu za hapo awali.

Wasafiri wa Marekani wataruhusiwa kuingiza bidhaa zenye thamani ya zaidi ya dola 400 zilizonunuliwa Cuba, kwa sababu za kibinafsi ikijumuisha Tumbaku na Pombe za thamani ya dola 100.

Kwa takriban miaka hamsini, Marekani na Cuba zimekuwa hazina uhusiano mzuri na kusababisha masharti mengi ya kibishara na usafiri.

XS
SM
MD
LG